Michezo

Barua nzito ya GSM kwa Yanga, yaanika makubwa bila kupepesa macho ”Tunawatakia kila lakheri” (+AUDIO) 

Sakata la Mdhamini wa Mabingwa wa kihistoria ligi kuu soka Tanzania Bara GSM dhidi ya Wanajangwani hao lafikia pabaya, kwa mujibu wa Wasafi FM, hii ndiyo barua iliyoandikwa na matajiri hao kwenda katika timu hiyo ya Wananchi Young Africans Sports Club.

BARUA YA GSM

MWENYEKITI,
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB,
P.O.BOX 15202,
DAR ES SALAAM.

Ndugu. YAH:MKATABA WA YOUNG AFRICANS SPORTA CLUB NA GSM TANZANIA LIMITED.

Husika na kichwa cha habari hapo juu. Kwa heshima na taadhima nachukua fursa hii kuushukuru uongozi mzima wa Klabu yetu ya YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB “YANGA” TIMU YA WANANCHI kwa ushirika wenu kwenye mambo kadha wa kadha kwenye kuirudishia heshima na kutatua changamoto nyingi zilizokua zinaikabili Klabu yetu.

Ikumbukwe kuwa changamoto nyingi ziliikumba na kuendelea kuikabili timu yetu na sisi tulijitahidi kuzitatua ingawa hazikua sehemu ya mkataba wetu.

NAZO NI

1.Kumrudisha LAMINE baada ya kutukatiza mkataba wake.
2.Kusajili wachezaji katika kuiongezea nguvu klabu yetu. I.Bernad Morisson. II.Ditram Nchimbi III.Haruna Niyonzima IV.Adeyum Saleh
3.Kuwaleta na kulipa gharama zote za KOCHA MKUU,KOCHA WA MAZOEZI NA VIUNGO (FITNESS COACH na PHYSIO)gharama hizo ni pamoja na mishahara, nusafiri wa ndani,nyumba na ticket za kwenda na kurudi makwao(BELGIUM & SOUTH AFRICA). 4.Kulipa Mishahara.
5.Kulipa Bonas za ushindi ktk mechi zote timu iliposhinda kuanzia Mwezi Desemba 2019.Pamoja na ahadi kubwa ya ushindi kwa mechi dhidi ya watani wa jadi na kuitekeleza
baada ya ushindi huo.

5.Kulipa gharama zote za CAMP/HOTEL kwa timu kuanzia mwezi Desemba 2019.

6.Tiketi za ndege kwa wachezaji na viongozi.

7.Kulipa na kugharamia uwanja wa mazoezi kwa ukamilifu wake.Hii ni pamoja na ukarabati wa uwanja na ununuzi wa vifaa vya mazoezi.

8.Kulipa baadhi ya madeni ya nyuma ya usajili wa wachezaji. Aidha,yote hayo yamekua yakifanyika kwa MAPENZI MEMA kwa klabu yetu bila kujali gharama nyingi na kubwa tunazolipa.

Pia,Katika kuelekea mabadiliko ya kiundeshaji wa Klabu,GSM ilitafuta wataalam( CONSALTANT)kuja kushauri na kusaidia mabadiliko ya kimfumo pamoja na kupata TIMU kubwa barani ULAYA itakayokuja kuwa ni TIMU RAFIKI katika kukuza maendeleo ya idara zote katika Klabu yetu CONSULTANT huyo yuko tayari na TIMU hiyo pia iko tayari kuja kuanza ushirikiano kwa Gharama za GSM.

Lakini,kumekua na malalamiko mengi sana kutoka kwa baadhi ya viongozi kuwa GSM imekua na ikiingilia majukumu yao na wao ndiyo wenye mamlaka hayo waliyokabidhiwa na WANACHAMA. Kwa masikitiko makubwa kauli hizi pia zimekua zikitekelezwa kwa vitendo

Usimamizi wetu umekua tu kwa yale tunayogharamia na kamwe hatukuwahi kutaka kujua mapato wala matumizi ya chanzo chochote cha Yanga.

Ikumbukwe pia, GSM imejitolea kwa hali na mali katika kuleta YANGA yenye maendeleo yake binafsi kupitia wanachama na KAMWE GSM haina nia ya KUPOKA MADARAKA WALA TIMU kutoka kwa mtu yeyote. YANGA NI WANANCHI NA ITABAKI KUWA YA WANANCHI

Kwa barua hi I,GSM itabaki kuwa mdhamini wa Yanga kimkataba na kutekeleza yale TU yaliyo Kwenye mkataba na kuachana na yote yaliyo nje ya mkataba.

Aidha,kwa niaba ya GSM tunaomba radhi kwa yoyote aliyekwazika na ushirika wetu katika kuijenga Klabu yetu na tuliyafanya hayo kwa mapenzi mema tu.

Tunawatakia kila la heri katika mapambano na tutaendelea kuwa sehemu ya mabingwa wa kihistoria.

DAIMA MBELE NYUMA MWIKO FOR GSM GROUP OF COMPANIES

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents