Burudani

Barua yamchanganya Shilole, atoa neno

Msanii wa Bongo Flava, Shilole amejikuta akisisimuka mara baada ya kupokea barua kutoka kwa mtoto wake ‘Rahma’.

Kupitia mtandao wa instagram Shilole ameweka barua ambayo ameandikiwa na binti yake huyo na kueeleza kuwa haamini jinsi amekuwa lakini katika yote hajutii kuwa mama.

Rahma binti yangu umeniliza na hii barua yako Siamim km Mungu amenikuzia kiasi hiki mpk leo katoto kangu ka pili kananiandikia maneno mazito hivi. Nakupenda sn mwanangu wewe na dada yako ndio urithi wangu na furahayangu….Nikivurugwa hukoo na ya ulimwengu nikitud nyumban nyio ndio faraja yangu.

Simkufuru Mungu kwa kuishi maisha ya shida niliyopitia, sisikitiki kwa kukosa elimu bora na kutimiza ndoto zangu nyingi nilizokuwa nazo nachojua MIPANGO YA MUNGU SIO KAMA YA MWANADAMU….Namshukuru kwa kila alichonipa, jina, umaarufu, rizki, marafiki na ndugu wa kweli lkn zaidi WATOTO wangu ambao kila iitwapo leo ndio mnanipa nguvu ya kuamka kupambana kuvumilia matusi vikwazo na kila vipingamizi. Nataka msome mtimize mdoto zenu nizeeke nikiona mnakuwa mabinti wa kuigwa na mumpendeze Mungu na wanadamu.

KAMA KUNA JAMBO NINAJIVUNIA KULIFANYA SAHIHI DUNIANI NA SIJAWAHI LIJUTIA NI MIMI KUKUBALI KUWA MAMA. By the way ndugu zangu sijui kizungu nimekielewa vizuri.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents