Burudani

Basata kuandaa tamasha la sanaa

 

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linajiandaa kufanya kongamano kubwa la muziki linalotarajiwa kufanyika  hivi karibuni ili kujadili mwenendo mzima wa fani hii ikiwa ni pamoja na kujenga utambulisho wa muziki wa Tanzania.

Ghonche Materego ambaye ni katibu Mtendaji wa BASATA alisema hayo jana kwenye  Ukumbi wa BASATA. Shughuli hiyo inaypotarajia kufanyika kila Jumatatu  itfafanua masuala mbalimbali yanayojitokeza kwenye Jukwaa la Sanaa na kusema kwamba,kongamano hilo pamoja na mambo mengine litakuja na majibu kadhaa ya changamoto mbalimbali zinazoikabili fani ya muziki nchini sambamba na kujenga heshima ya wasanii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

Awali Ghonche alisema, ‘Tunakusudia kufanya kongamano kubwa ambalo litahusisha maproducer, wadau wa vyombo vya habari, mapromota, wasanii wote wa muziki na wadau mbalimbali wa sekta ya sanaa ili kwa pamoja tujiulize fani yenyewe iendeshwe vipi na tutajengaje utambulisho wa muziki wetu ili tuweze kuuzika kimataifa   alisisitiza Materego.

Aliongeza kwamba, muda umefika sasa kwa wasanii wa muziki na wadau wote kukaa chini na kukuna vichwa juu ya mwenendo mzima wa fani hii kwani kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiibuka na kuzua wasiwasi wa fani hii kudidimia na kukosa muelekeo kama jitihada za makusudi hazitafanyika.

Alihoji tabia inayokua kwa kasi ya baadhi ya wasanii wa kitanzania kunakiri vionjo (beats) vya miziki kutoka nje hasa Marekani na kuonyesha wasiwasi wa wasanii wetu kuja kuburuzwa mahakamani na hata kutozwa faini kubwa za fedha kutokana na kitendo hicho kukiuka sheria za kimataifa za hakimiliki na hakishirikishi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents