Burudani

BASATA lampa Rosa Ree mwezi mmoja kulipa faini ya kiasi hiki cha fedha

Baraza la Sanaa la Taifa “BASATA”  limempunguzia adhabu rapa wa kike nchini, Rosa Ree kutokana na kumfingia miezi sita, na badala yakekuruhusiwa kuendelea na shughuli zake za kisanaa.

Barua hiyo imemtaka msanii huyo kulipa ffaini ya shilingi Milioni 2 ndani ya muda wa mwezi mmoja,

“Baraza la sanaa la Taifa linapenda kukutaarifu kuwa ombi lako la kupunguziwa adhabu limekubaliwa baada ya kujutia kosa lako na kumuandikia barua Mh. Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo ili kuomba kupunguziwa adhabu”, Barua kutoka Basata.

Aidha barua hiyo iliendelea kusema “1. Kuanzia tarehe ya barua hii, unaruhusiwa kuendelea na shughuli za sanaa, hivyo adhabu uliyopewa ya kufungiwa miezi 6  imeondolewa, 2. Kulipa faini ya milioni 2, kama ulivyoagizwa na hii ilipwe ndani ya mwezi mmoja”.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram Rosa Ree ameandika “Napenda kutoa shukrani kwa ofisi ya Waziri wa sanaa, habari, utamaduni na  michezo Mhe. Harrison Mwakyembe na BASATA, kwa kuniruhusu kuendelea kufanya shughuli zangu za sanaa, naahidi kufanya kazi zangu ipasavyo na kuendelea kuipeperusha bendera ya nchi yangu”

Ikumbukwe mwezi uliopita Basata walimfungia Rosa Ree kwa muda wa miezi sita na kumtaka alipe faini ya Milioni 2, kwa makosa mawili ambayo ni kuachia video iliyokosa maadili pamoja kufanya kazi nje ya nchi bila kuwa na kibali.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents