Burudani

BASATA wafunga mafunzo ya sanaa kwa watoto 100 wa shule za msingi

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limefunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kisanaa kwa wanafunzi 100 wa shule nne za msingi ambazo ni Kizimzumbwi, Kibasila, Sanze, Nyanzige A pamoja na Nyanzige B kutoka wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani.

Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Msoko, BASATA, Nsao Vivian Shalua (kulia), Afisa Elimu Kisarawe, Zipporah Daniel Simwanza (katikati) na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya, Simon John Biginagwa (kushoto).

Mafunzo hayo yalikuwa ni kwaajili ya kuwajengea uwezo wanafunzi katika sanaa wanazofanya pamoja na kukuza vipaji vya watoto hao.

Watoto hao walifundishwa kuimba nyimbo za asili, kucheza ngoma pamoja na kupewa njia mbalimbali ambazo zitafanya wa-ballance masomo yao ya darasani pamoja na sanaaa zao.

Akiongea katika sherehe hiyo, Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Msoko, BASATA, Nsao Vivian Shalua alisema lengo la mafunzo hayo ni kukuza vipaji vya watoto na kuendeleza sanaa kwa wototo na kufufua Sanaa ya ngoma.

“Hapo awali masomo ya sanaa yalifundishwa katika shule za msingi hivyo wanafunzi waliweza kupata fursa ya kuonyesha sanaa kama vile maigizo, majigambo na kucheza ngoma za asili za kijamii, ubunifu, uchangamfu wa kupenda shule aidha walimu walikuwa wakifundisha kwa kutimia njia ya sanaa hivyo kurahisisha ufundishaji na ufaulu kuwa mkubwa,” alisema Shalua.

Aliongeza,”Sanaa ni mojawapo ya kipengele cha Utamaduni lakini somo la sanaa kwa sasa limeonekana kutopewa kipaumbele badala yake kuwa somo la ziada matokeo yake Tanzania linaelekea kuwa taifa mfu lenye kuiga tamaduni za nchi nyingine na hivyo kubeba roho ya matiafa mengine. Mafunzo haya wawechachu ya kuimarisha na kuhamasisha sanaa mashuleni na kupelekewa watoto wengi kupenda shule,”

Walimu akiwa pamoja na wanafunzi hao

Shalua alitoa wito kwa Halmashauri ya Kisarawe kuimarisha kamati za sanaa ili kukuza na kuendeleza maendeleo ya sanaa katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vikundi na wadau wote wanaofanya kazi za sanaa kusajiliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Naye Afisa Elimu Kisarawe, Zipporah Daniel Simwanza alisema mafunzo hayo yataweza kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa kufanya vizuri darasani kwa kuwa wanapata burudani pamoja na kujifunza kwa wakati mmoja.

Akiongea katika ukumbi huo, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya, Simon John Biginagwa alisema ofisi ya mkuu wa wilaya kupitia ofisi ya Maendeleo ya Sanaa wilayani huyo itajenga kituo cha sanaa ambazo kitawaaidia wakati wa wilaya hiyo kujifunza sanaa na kupata sehemu ambayo itakuwa ni mlezi wa sanaa.

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya, Simon John Biginagwa

Afisa Elimu Kisarawe, Zipporah Daniel Simwanza

Picha ya pamoja

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents