Burudani

BASATA wakanusha kumuita na kumhoji Wema Sepetu “kama ni mambo ya mtandao labda TCRA”

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limekanusha taarifa ambazo zinazagaa mtandaoni kwamba wamemuita malkia wa filamu Tanzania, Wema Sepetu kutokana na kusambaza video mtandaoni akila denda na mwanaume aliyedai ni mpenzi wake mpya.

Wiki iliyopita muigizaji huyo aliachia video hiyo na picha za mwananume huyo akidai ameshindwa kulizuia penzi lake hilo kwa mwanaume huyo.

Baada ya kugaa kwa taarifa hizo, Bongo5 ilizungumza na Afisa Habari Basata, Agness na kukanusha taarifa hizo huku akidai kama mwanadada huyo anaenda Basata ni kwa mambo yake binafsi sio kwamba aliitwa.

“Sio kweli Wema ameitwa Basata, hata sisi tunasikia hizo habari na kuihusisha na mambo yake ya kwenye mitandao, sisi kama Basata atu-deal na maisha binafsi ya wasanii labda afanye tukio katika kazi ya sanaa ndio tunaweza kumuita,” alisema Agnes “Kama ni mambo ya mtandaoni TCRA ndio wenye mamlaka,”

“Basata ni sehemu ya wasanii, ni wazazi wa wasanii, kama anakuja sisi tutampokea na kuzungumza naye hukusu sanaa yake na namna ya kujiweka kama msanii lakini mpaka sasa hatuna taarifa kama anakuja lakini akija sawa tutampokea,”

Mpaka hakuna taarifa rasmi kwamba mrembo huyo ameitwa na jeshi la Polisi kwaajili ya tukio hilo au la!.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents