Burudani

Bashiri shabiki mkubwa wa albam mpya ya Jay Z ‘MCHG’…. Ni Blue Ivy

Anaweza kuwa na umri wa miezi 18 tu lakini Blue Ivy tayari ni shabiki wa muziki wa baba yake, Jay Z.

article-2440454-186ECD5300000578-328_634x627

Jay mwenye miaka 43, amesema binti yao huyo na Beyonce anapenda kusikiliza albam mpya ya baba yake, Magna Carta… Holy Grail.

“Anapenda nyimbo zote,” Jay aliliambia jarida la Vanity Fair kwenye interview yake mpya.

article-2440454-186EBAF900000578-231_634x877

“Hucheza wimbo na kusema, ‘More, Daddy, more… Daddy song’ ni shabiki wangu mkubwa. Kama kusingekuwa na mtu aliyenunua Magna Carta, ukweli kwamba anaipenda, inanipa furaha kubwa.”

“Sijui kama Blue alishawahi kusikia muziki wangu kabla ya albam hii. Huwa sichezi muziki ndani ya nyumba,” aliongeza.

Jarida hilo litatoka mwezi November.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents