Habari

BASI la kanisa lakamatwa likisafirisha misokoto ya bangi Kenya

Basi la kanisa la Kipentekoste la PEFA limekamatwa mjini Voi nchini Kenya likisafirisha madawa ya kulevya aina ya bangi.

Kwa mujibu wa Polisi mjini humo, Bernastein Shali,  amesema kuwa wanawashikilia watu watatu akiwemo dereva wa gari hilo.

Kamanda Shali, amesema basi hilo lilikuwa limesafirisha waombolezaji kutoka Mjini Kilifi kwenda Homa Bay na wakati wa kurudi lilipakia bangi hiyo.

Polisi wamesema tukio hilo, Limetokea Jumanne ya wiki hii kwenye barabara ya Nairobi-Mombasa, Na wamekamata misokoto 230 yenye zaidi ya thamani ya Tsh. milioni 1.5 .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents