Michezo

Basi la wachezaji wa Maji Maji FC lawekwa bondi hotelini/ wakopeshwa hadi nauli ya kuridi kwao Songea/ zabaki siku tano za kuligomboa 

Klabu ya Maji Maji FC yenye maskani yake Mjini Songea Mkoani Ruvuma imejikuta ikiweka basi lake ‘bondi’ kufuatia madeni wanayodaiwa na hoteli ya JM iliyopo jijini Dar es salaam.

Maji Maji inaonekana kukabiliwa na ukata wa hali ya juu hali iliyopelekea kushindwa hata kulipia hoteli wanayofikia pindi wanakuwa Dar es salaam na kupelekea kulimbikiza madeni hadi kufikia kuwa kubwa na hivyo kuliweka kwa mkopo basi la wachezaji wao.

Meneja wa JM Hoteli, Emmanuel Mapolu amekiri kuwadai wateja wake hao kiasi cha zaidi . ya milioni mbili wakati walipokaa hapo wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya timu ya Friends Rangers mechi ya ligi daraja la kwanza.

”Tunawadai milioni tatu la elfu tisini ambalo ni deni lao lote, deni lenyewe lilikuwa ni milioni mbili na tisi lakini tukawapa milioni moja kama hoteli ili waweze kufanya nauli waweze kuondoka na basi waliache hapa,” amesema meneja huyo wa hoteli ya JM, Emmanuel Mapolu.

Emmanuel Mapolu ambaye ni meneja wa JM Hoteli ameongeza ”Watakapokwenda kujipanga huko watafute pesa yetu waje watulipe, wachukue basi lao, tarehe 8/ 05/ 2019 ndiyo mwisho wanatakiwa kuwa wameshalilipa deni hilo.”

Meneja huyo ameongeza kuwa hoteli imewapa uongozi wa Maji Maji FC muda wa wiki mbili ili waweze kugomboa basi hilo na kama itashindikana wataangalia hatua nyingine za kisheria.

Bongo5 imemtafuta meneja wa klabu ya Maji Maji, Godfrey Mvula na kufanya naye mazungumzo juu ya deni hilo lililopelekea hadi kuweka ‘bondi’ basi la wachezaji.

”Ni kweli tumeliacha kwakuwa tunadaiwa milioni tatu na tisini lakini kimsingi tumeshaanza kupunguza deni hilo lakini kabla ya tarehe ya ‘dead line’ tutakuwa tumeshaligomboa,” amesema meneja wa klabu ya Maji Maji, Godfrey Mvula.

Klabu ya Maji Maji ilikabidhiwa basi hilo na Mbunge wa jimbo la Songea Mjini, Dk. Emmanuel John Nchimbi ilipofanikiwa kurejea ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa mwaka 2017/18 ambapo Dk Nchimbi alimshukuru rafiki yake, Paul Hinks kwa kufanikisha kupatikana kwa gari hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents