Tragedy

Basi laua 7, lajeruhi 30

Watu zaidi ya saba wanasadikiwa kufa papo hapo na wengine 30 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya basi kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Bahi, Dodoma.

Na Mary Edward,PST Dodoma

 
Watu zaidi ya saba wanasadikiwa kufa papo hapo na wengine 30 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya basi kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Bahi, Dodoma.

 

Ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Air Bus mali ya kampuni ya Tashrif lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Singida.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Bw. Omar Mganga, aliiambia PST kuwa alikuwa hajapata idadi kamili ya watu waliokufa lakini ametuma kikosi cha polisi na taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo ataitoa leo.

 

Abiria walionusurika katika ajali hiyo, walisema ilitokea wakati basi hilo likiwa katika mwendo wa kasi huku likijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake wakati huo huo kukiwa na lori lingine lililokuwa kwenye mwendo wa kasi likija na kugongana uso kwa uso.

 

Abiria hao walisema watu zaidi ya saba wanasadikiwa wamekufa papo hapo na kwamba abiria wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa vibaya.

 

PST ilishuhudia majeruhi na maiti kadhaa wakifikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma huku majeruhi watano akiwemo mwanaume mmoja wakiwa katika hali mbaya.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents