Michezo

Bastian Schweinsteiger kufungiwa na FA

Kiungo wa Manchester United, Mjerumani Bastian Schweinsteiger 31, anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa mechi tatu na chama cha soka England (FA) kutokana na kitendo chake cha kumpiga kiwiko mlinzi wa Westham United, Winston Reid katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana Jumamosi iliyopita.

wes

Schweinsteiger anatakiwa hadi Alhamis hii, saa sita mchana kukubali au kukataa kosa hilo baada ya FA kumuadhibu Jumatatu hii.

FA-Rungu-1

Chama cha waamuzi kupitia video wamebaini kosa hilo la Bastian Schweinsteiger lililotokea kabla ya mapumziko na sasa mchezaji huyo anaweza kufungiwa hadi mechi tatu zinazosimamiwa na chama cha soka England, FA.

Habari hizi sio nzuri kwa Manchester United ambayo inakabiriwa na majeruhi ya viungo wake kama Morgan Schneiderlin na Ander Herrera huku Bastian Schweinsteiger akiwa miongoni mwa watu muhimu katika kikosi hicho hivi sasa.

Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal akizungumzia tukio hilo anasema hakuona chochote na hivyo hana la kufanya zaidi ya kuwaachia wenye mamlaka kutimiza sheria.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents