Burudani

Baucha kuanzisha ‘mobile studio’ kurekodi na wasanii wa mikoani

Producer na msanii Baucha amesema amedhamiria kuanzisha mobile studio ili kuweka unafuu na urahisi wa ufanyaji kazi kwa wasanii wa mikoani na wilayani ambao walikuwa na ndoto ya kufanya wimbo/nyimbo kwenye studio kubwa Tanzania.

11373922_886987541387086_413510208_n

Katika mahojiano aliyoyafanya na mtangazaji Ergon Elly wa Kitulo FM – Njombe, Baucha alisema wasanii wengi kutoka mikoani wanatamani kuja Dar es Salaam kwaajili ya kurekodi kazi zao lakini kutokana na gharama za kuendesha maisha kwa kipindi chote cha kurekodi ina hivyo wengi wemekuwa wakishindwa kutimiza ndoto zao katika muziki.

Baucha Records na timu nzima ya Baucha inatarajia kuanza kufanya kazi (Mobile Studio) katika mikoa mitatu ya kusini mwa Tanzania ambayo ni Njombe,Mbeya na Iringa na baadaye mikoa mingine ya Tanzania.

Watayarishaji wengine wa muziki waliowahi kuwa na wazo hilo ni Man Water wa Combination Sound na Mr T wa Free Nation.

Unaweza kusikiliza mahojiano hayo hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents