Burudani

Baucha: Wasanii wa Tanzania wajitangaze zaidi kimataifa

Producer mkongwe anayejulikana zaidi kwa kusaidia kumtoa Fid Q na wimbo wa Fid Q.com uliorekodiwa kwenye studio yake, Ally Baucha ameongea na bongo5 na kusema kimya chake kilitokana na yeye kusafiri lakini pia kumwachia studio mtu ambaye yeye anafikiri hakuwa serious katika shughuli hiyo.

Baucha anasema anadhani kikubwa kilichosababisha mtu wake kushindwa kuiendeleza studio ni ushindani mkubwa uliopo pamoja na mabadiliko ya teknolojia kwa upande wa softwares na vitu vingine vya upande huo na hivyo ilibidi ampumzishe wakati akipanga mkakati wa kurudi tena.

Akiendelea Baucha anasema kwa sasa pamoja na kwamba amerudi tena lakini pia anampika produsa mwingine ambaye amemtaja kwa jina la Jose a.k.a Sumu aliyetengeneza wimbo wake mpya uitwao “Kelele” aliyomshirikisha Ali Kiba.

Baucha anasema kwa sasa studio yake inatengeneza nyimbo aina mbalimbali kuanzia bongo flava, gospel, Rhumba, Taarabu n.k.

Kuhusu muziki wa Tanzania Baucha alisema katika kutengeneza muziki hapa Tanzania kuna makosa madogo madogo ambayo hata katika nchi zilizoendelea yapo na siyo kitu cha kumkatisha tamaa hivyo kusisitiza dhamira ya kufanya kazi kwa moyo wote bila kuchoka.

Akiongelea namna ambavyo analiona game tangu alivyopotea, Baucha amesema kwa sasa muziki wa Bongo unafanya vizuri lakini anafikiri kuna mkazo ambao unatakiwa kuwekwa kwa wasanii wa kitanzania kujitangaza zaidi nje ya nchi.

“Ki ufupi kuna maeneo mbali mbali ambayo tumeendelea ama tumesogea kidogo kwa sababu teknolojia inatubeba kiasi, ingawaje kwenye upande wa production ama utayarishaji tumerudi nyuma kwa sababu teknolojia iliyopo ni ya kibiashara zaidi na tasnia iko wazi yaani mtu yeyote anaweza kuingia na kufanya kile ambacho anataka kufanya hivyo na pia serikali ilikuwa haijafanya jambo lolote kukabiliana na hilo la kuhalalisha tasnia kuwa sekta rasmi, ingawaje najua ikifika mwezi wa kwanza mambo yote hayo yatabadilika kwani bunge letu lilishaanza mchakato huo kitakachofanyika ni kupitisha rasmi,” alisema.

Baucha alisema kazi yake mpya inaitwa Kelele na pia amemshirikisha Alikiba kwa sababu wote wawili ni washkaji wa siku nyingi lakini pia kwa kufanana kwa kwa jina la Ally na pia kwa kuwa Ally ameshatoka kimataifa kwa hiyo itakuwa rahisi kwake kukubalika pia katika soko jingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents