AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Bayern Munich yanasa saini ya Benjamin Pavard aliyetisha kombe la Dunia

Klabu ya Bayern Munich imefikia makubaliano ya kumsaini beki wa Kimataifa wa Ufaransa, Benjamin Pavard kwa mkataba wa miaka mitano utakao anza msimu ujao hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo, Hasan Salihamidzic.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atajiunga na miamba hiyo ya soka ya Bundesliga akitokea VfB Stuttgart huku akiwa ni sehemu ya wachezaji waliyofanikiwa kucheza michuano ya kombe la Dunia mwaka 2018 na kuchukua kombe akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa ambapo alifanikiwa pia kutupia bao bora kabisa dhidi ya Croatia.

Usajili wake umegharimu kiasi cha pauni milioni 31.4 ambapo sawa na euro milioni milioni 35.

“Ninatangaza kwamba tutaanza kupata huduma ya Benjamin Pavard kuanzia Julai 1 mwaka 2019, mkataba wa miaka mitano,” amesema Salihamidzic.

Salihamidzic amethibitisha kuwa Bayern inampongo wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Callum Hudson-Odoi ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji akiwemo mawinga wao, Arjen Robben na Franck Ribery mwishoni mwa msimu.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW