Burudani

Hannington ampiga Lerato, atimuliwa BBA

Katika kitendo kilichowastaajabisha wadau wengi wanaotazama Big Brother, Hannington kutoka Uganda alimpiga kibao Lerato kutoka South Africa,kitendo ambacho kimesababisha atimuliwe katika jumba hilo la Big Brother.

 

Ugomvi huo ulitokea pale ambapo Lerato alimuuliza Hanningto swali lililomkera na kumlazimisha kujibu. Hanningtona laionekana kupandwa na jazba na kumsukuma Lerato ukutani na baada ya mwanadada huyo kujaribu kumsukuma na chupa ya pombe ndipo Hannington alimzaba kibao hicho.Sheila kutoka Kenya ndiye alikimbia na kuamua ugomvi huo pasipo kuendlea kuwa mmbaya.

Big Brother alimuita Lerato ili amsikilize na kutaka kujua zaidi kilichoendelea. Lerato alisema hajawahi kupigwa na mtu yeyote hata wa familia yake na alijisikia kudhalilishwa sana na kitendo hicho. Aliapa kutosahau kitendo hicho cha Mganda huyo kumpiga ingawa atamsamehe. Alisema asingependa kuongea naye tena.

Hannington aliomba msamaha na hata kufikia kitendo cha kutaka kuondoka katika jumba hilo la Big Brother kwa kile alichosema ni kitendo cha aibu alichofanya.Big Brother aliamua kumondosha na kumrudisha nyumbani Kijana huyo.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents