Burudani

BBA: Prezzo azidi kupeta


Jana mshiriki wa Uganda Janette alifungasha virago kwenye shindano la Big Brother Africa Stargame. Jina la kwanza kutajwa kwenye live eviction show lilikuwa la Prezzo lakini haraka ikawekwa wazi kuwa mfalme huyo wa pamba bado anabaki mjengoni.
Kutokana na matokeo hayo, Prezzo anazidi kuongeza matumaini ya kuchukua kitita cha dola laki tatu kitakachotolewa kwa mshindi wa mwaka huu.
Baada ya kubainika kuwa mshiriki huyo wa Kenya ameokoka dhidi ya mkasi wa kutolewa, mitandao ya kijamii hususan Twitter ilikuwa busy kwa shangwe juu ya habari hiyo njema.
“Prezzo is the man to take the price…he has all qualities!” aliandika mfuatialiji wa mashindano hayo.
“PREZZO is safe, we should not worry,we just have to prepare troops 4 next week finale,” aliandika mwingine.
Na sasa imebaki wiki moja tu hadi kufikia kilele cha shindano hilo, huku wakati huu watu wakianza kumpigia kura mshindi wa BBA Stargame.
Uhakika wa zawadi hiyo kuja Afrika Mashariki ni mkubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents