DStv Inogilee!

BBA The Chase: Afrika Mashariki yamuokoa Annabel wa Kenya, na Afrika yawapa tiketi Selly na Natasha

Msimu wa 8 wa reality show inayoiunganisha Africa kupitia Big Brother ‘The Chase’ ukiwa unaendelea, idadi ya washiriki inazidi kupungua kadri ya siku zinavyozidi kwenda na jana ilikuwa ni zamu ya washiriki wa Malawi na Ghana kufungasha mizigo yao.

selly n natasha
Selly & Natasha

Wakiwa wamedumu kwa wiki 7 katika mchezo hatimaye eviction show ya jana (July 14) iliwapa tiketi Natasha (Malawi) na Selly (Ghana) walioshindwa kupata kura za kutosha kuwafanya waendelee kuiburudisha Afrika.

Selly ndiye aliyepata kura ndogo zaidi kati ya washiriki wote sita waliokuwa danger zone kwa kura moja tu ya nchi yake Ghana. Natasha, Pokello na Cleo waligongana kwa kupata kura mbili mbili hivyo ulitumika utaratibu wa kuangalia aliyepata asilimia ndogo zaidi kwa kura za nchi zote na bahati mbaya ilidondokea kwa Natasha wa Malawi.

Africa mashariki inaendelea kuonesha umoja kwa kuwapigia kura washiriki wao ambapo wiki hii kura za Kenya, Uganda na Tanzania ndio zimemuokoa Annabel muwakilishili wa Kenya aliyepona kwa kura 3.

votes week 7

Hivi ndivyo Afrika ilivyopiga kura:

Angola: Melvin
Botswana: Cleo
Ghana: Selly
Kenya: Annabel
Ethiopia: Natasha
Malawi: Natasha
Namibia: Melvin
Nigeria: Melvin
South Africa: Pokello
Sierra Leone: Melvin
Tanzania: Annabel
Uganda: Annabel
Zambia: Cleo
Zimbabwe: Pokello
Rest of Africa: Melvin

Jumla: Melvin = 5; Annabel = 3; Cleo = 2, Pokello = 2, Natasha = 2, Selly = 1. (Jumla: 15 Votes)

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW