Burudani

BBA The Chase: Annabel, Bolt na Natasha waingia tena danger zone, Nando ajiokoa mwenyewe

Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo washiriki wa ‘tricky game’ Big Brother Africa The Chase wanazidi kupungua na mchezo ndivyo unazidi kuwa mgumu kwa wale wanaofanikiwa kubaki, sababu idadi inavyozidi kupungua ndivyo nafasi ya kila mshiriki kupigiwa kura ya kutoka inavyozidi kuongezeka.

the chase

Ikiwa ni wiki ya 5 tayari washiriki 7 wameshajifahamu kuwa wamechaguliwa kuingia katika possible eviction ya Jumapili (June 30), na kati yao washiriki wanne wameingia tena kwa mara nyingine baada ya kuponea chupu chupu wiki zilizopita.

Annabel mshiriki pekee wa Kenya aliyebaki mchezoni , Bolt wa Sierra Leone ambaye sasa anaendelea na mchezo bila mpenzi wake Betty aliyetolewa Jumapili iliyopita, na Natasha wa Malawi wameingia kwa mara nyingine tena wiki hii baada ya kufanikiwa kuokolewa na kura za Wa Afrika.

Baada ya Nando wa Tanzania kupona katika eviction ya Jumapili iliyopita kwa kupigiwa kura na nchi 5, jana alipigiwa kura ya kuingia tena katika possible eviction ya wiki hii, lakini alitumia vizuri nafasi yake ya ukuu wa nyumba (HOH) wa Diamond na kujiokoa na nafasi yake akampa Maria wa Namibia.

Wengine ambao wameingia katika kikaango cha wiki hii ni Pokello wa Zimbabwe, Dillish wa Namibia, na Hakeem wa Zimbabwe.

Jumapili ya (June 30) tutashuhudia washiriki wengine wawili kati ya hawa saba watakaouaga mchezo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents