Burudani

BBA The Chase: Beverly amuokoa Bimp na kumuweka Dillish kikaangoni

Jana Jumatatu ilikuwa ni siku ya nomination katika big brother na majina yaliyopata kura nyingi yaliongozwa na Feza wa Tanzania aliyeongoza kwa kura 4 akifuatiwa na Bimp na Cleo waliopata kura 3 kila mmoja.

THE CHASE LOGO

Kilichokuwa kinasubiriwa ni HOH kutumia nafasi yake ya kumuokoa mshiriki mmoja aliyeingia katika nominations kwa kumuweka mwingine, na mnigeria Beverly anayeiongoza nyumba wiki hii aliamua kumuokoa kipenzi cha wengi kwa sasa Bimp na nafasi yake kumuweka mrembo Dillish.

Hivyo washiriki watatu ambao wako kikaangoni wiki hii ambao imetokea kuwa wote ni wasichana ni Feza (Tanzania), Dillish (Namibia) pamoja na Cleo (Zambia).

Je unadhani kuondoka kwa Bimp katika kikaango cha wiki hii kutasaidia kuongeza kura za kumuokoa Feza kutokana na kuwa mshindani mkubwa Bimp yuko salama? Kura yako inahitajika kumuokoa Feza anayeipeperusha bendera ya Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents