Burudani

BBA The Chase: Majina ya wasanii watakaolipamba jukwaa la ‘The Chase’ siku ya fainali yafahamika

Leo ni siku ya 89 katika kalenda ya BBA, zimesalia siku mbili tu kabla ya msimu wa nane wa Big Brother Africa ‘The Chase’ kufikia ukingoni na tayari majina ya wasanii watako pamba jukwaa la fainali za shindano hilo yameshafahamika.

Ice Prince-2
Ice Prince

Star wa Nigeria Ice Prince pamoja na Keko kutoka Uganda ni miongoni mwa wasanii waliopewa jukumu la kusindikiza fainali hizo katika upande wa burudani, wakiwa wanatarajiwa kuwarusha housemates na wote watakaohudhuria katika tukio la kuweza kumfichua mshiriki atakayepewa idhini na Waafrika kuondoka na $300,000 ya mshindi wa The Chase.

KEKO

Wasanii wengine watakaomiliki jukwaa siku hiyo ni pamoja na DJ Ganyani wa Afrika Kusini pamoja na kundi la R2bees kutoka Ghana.

Beverley, Melvin, Elikem, Cleo na Dillish ndio Top 5 iliyofanikiwa kuingia fainali ambayo itatoa majibu ya mshindi siku ya Jumapili hii (August 25) kuanzia saa 1 jioni kupitia DSTV.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents