Burudani

BBA Updates: Washiriki wapigana vikumbo kuingia Top 5, Elikem apigiwa kura nyingi za kuingia dangerzone!

Reality Show ya Big Brother Africa msimu wa nane uliopewa jina la ‘The Chase’ sasa ndio uko katika hatua ngumu zaidi kwa washiriki wote saba ambao kila mmoja anahitaji kutumia akili ya ziada ili kufanikiwa kuingia tano bora itakayoenda fainali wiki ijayo.

the chase

Nomination kwaajili ya possible eviction ya mwisho wiki hii tayari imefanyika leo Jumatatu na Elikem ambaye ameshakuwa na tiketi ya kuingia fainali ndiye (mti wenye matunda) anayeongoza kwa kupendekezwa zaidi.

Mnigeria Beverly ambaye hajawahi kuingia katika dangerzone ndiye aliyekuwa wa kwanza kupiga kura yake na kumpendekeza Cleo pamoja na Dillish. Kama wasemavyo malipo ni hapa hapa Cleo naye baada ya kuingia dairy session aliwachagua Beverly na Elikem waingie dangerzone, huku akitoa sababu za kumpendekeza Bev kuwa hajawai kupendekezwa kutoka hivyo anataka kupima uwezo wake, na Elikem sababu ni HOH hivyo anajua atajiokoa.

Dillish alimchagua Elikem kwa sababu kama za Cleo kwamba kwasababu ni HOH, na akamchagua Bimp kwasababu anaonekana kuwa na upinzani mkubwa kwake.

Bimp naye amempendekeza Dillish kwa sababu pia anaihisi kuwa anampa upinzani mchezoni, na kura yake ya pili ikamwendea Elikem kwasababu hawana maelewano mazuri toka wakati tukio la Nando.

Upande wa HOH Elikem aliyerushiwa risasi nyingi za kutoka naye alimpendekeza Bimp kwa sababu za kutokuelewana kwao, na pia amempendekeza Angelo. Angelo naye amempendekeza Elikem akiamini ana nafasi ya kujiokoa wakati Melvin ambaye leo hajapendekezwa kabisa yeye kura zake zimemwendea Bimp na Elikem .

Usiku wa leo mkuu wa nyumba mghana Elikem atakuwa na wakati mgumu wa kufanya maamuzi ya mshiriki wa kumpendekeza ili kuziba nafasi yake lakini kwa umakini wa kumuondoa yule ambaye hatampa upinzani mkubwa zaidi katika fainali.

Hivi ndivyo mapendekezo ya leo yalivyokuwa:

Elikem: 5
Bimp: 4
Dillish: 2
Cleo: 1
Beverly :1
Angelo: 1
Melvin: 0

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents