Habari

BBC yaomba radhi kwa kuonesha video yenye picha ya Prince William wa Uingereza akiwa amechorwa ‘nyeti’ za kiume usoni (video)

Shirika la habari la Uingereza BBC limeomba radhi kwa kile wanachodai kuwa walionesha kwa bahati mbaya video yenye picha ya Prince William wa Uingereza ikiwa imechorwa nyeti za mwanaume katika uso wake.

prince-3

Inadaiwa kuwa siku ya Alhamisi asubuhi (August 1) kituo cha TV cha BBC kilirusha video ya wimbo “I Could Have Married Kate” ya kikundi cha muziki cha Comedy kiitwacho ‘Barbershopera’ bila wao kugundua katika video hiyo kuna picha inayomdhalilisha Prince William iliyochorwa nyeti za mwanaume katika uso wake.

Watazamaji ndio waligundua picha hiyo na kuanza kutweet kuhusiana na walichokiona.

price-2

Baadae BBC waliomba radhi kwa kusema ‘Barbershopera’ waliwaletea video hiyo na kwa bahati mbaya maproducer wao hawakugundua kasoro hizo mapema.

“the material was provided by Barbershopera but we failed to spot the offending material within it. We apologize for this.” BBC waliomba radhi mchana wa siku hiyo.

Tazama video hiyo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents