DStv Inogilee!

BBC yazindua kipindi kipya cha afya ‘BBC Maisha’

BBC Maisha kipindi kipya cha Afya kinazinduliwa wiki hii kwenye runinga yako, na kinaangazia masuala ya afya ambayo mara nyingi huonekana kama mwiko, japo yanaendelea kuathiri jamii Barani Afrika. Kipengele cha kwanza kwa jina FUNGUKA kinatoa nafasi wachangiaji na jamii nzima kufungua siri zao katika maisha ambazo mara nyingi zinagusa afya na maisha yao .

Makala ya kwanza yanaagazia utamaduni wa kuwakeketa wanawake na wasichana . Ni suala muhimu sana hususan msimu huu wa likizo ndefu, ambayo kuna mambo mengi yanafanyika katika jamii, moja wapo ni watoto kupelekwa jandoni, baadhi ya jamii zikiwakeketa wasichana wao. Makala mengine yajao yataangazia tatizo la kutoa/kuavia mimba, Sonanoa, Huzuni, uraibu wa mihadarati, na unyaji pombe wa kupindukia.

Mtangazaji nyota wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Maryam Dodo Abdullah ndiye anayeongoza mazungumzo ya FUNGUKA, akiwa na ufasaha wa lugha na uwelewa masuala ya afya hususan kanda ya Afrika Mashariki.

Mhariri wa kipindi cha BBC MAISHA Anne Mawathe, anataja kipengele cha FUNGUKA kama nafasi muhimu sana ya kuongea wazi kuhusu masuala aya afya ambayo mara nyingi jamii hopuuza na mara nyingi waathiriwa wakiishi kwa unyanyapaa. FUNGUKA inaangazia mambo mazito na ambayo wakati mwingine jamii haitaki kuyazungumza, kwa kuyatoa yaliyo moyoni jamii inaanza kujinasua na kujadili masuala ya afya, na hatimae hata kutafuta suluhu.

BBC Maisha inapeperushwa kupitia Runinga Washirika

· Star TV (Tanzania) – Alhamisi saa moja jioni. Marudio ni Jumapili saa Saba Adhuhuri

· KBC (Kenya) – Jumamosi saa Mbili Jioni

· Pia unaweza kutizama kwenye mitandao yote ya @BBCSwahili.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW