Michezo

Beckham apewa onyo

 

David Beckham ameonywa kesi ya madai ya paund milioni 16 (shilingi bilioni 32) aliofungua dhidi ya changudoa Irma Nici huenda ikamgeukia mwenyewe.

Wakili wa Irma, Paul Jensen, akisema changudoa huyo atatoa ushahidi unaoonyesha alifanya mapenzi na nyota huyo wa England.

Irma raia wa Bosnia alisema anauhakika Beckham alimlipa fedha kwa ajili ya kufanya naye mapenzi na aliongeza kuwa baada ya kesi atahitaji kulipwa fidia.J ensen alisema Beckham atajutia kosa la kumshtaki msichana huyo kwani mambo mengi yatangundulika.

Wakili huyo aliongeza kuwa mambo yatakayo wekwa wazi hayatashangaza watu wengine pekee bali hata mwenyewe Beckham.

Jensen alidokeza kuwa wakati Beckham anamchukua Irma alimfanyia mambo mabaya ikwa ni pamoja na kumdhuru mwilini. Kesi ya Irma na Beckham itaazwa kusikilizwa rasmi Februari16 mwakani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents