Burudani

Beef? Kanye West aondoa neno ‘Jay Z’ kwenye mashairi ya nyimbo zake 3 wakati wa live performance

Kama ulidhani Kanye West alichukulia poa Jay Z na Beyonce kuipotezea harusi yake na Kim Kardashian mwezi uliopita, basi fikiria upya kwakuwa Yeezy alimind.

Kanye West na Jay-Z wakipokea tuzo

Weekend iliyopita West aliziongezea nguvu fununu za kuwepo kwa beef kati ya washkaji hao wakati akitumbuiza X Games huko Austin, Texas. Wakati akiimba nyimbo tatu za mwisho, Kanye aliondoa jina Jay kwenye mashairi yake ya kawaida.

Kwenye wimbo wake Cold, West hurap “Lucky I ain’t had Jay drop him from the team.” Badala yake alilitoa jina “Jay” na kuacha beat peke yake.

Kisha kwenye Blood on the Leaves, pia aliacha jina la Jay kwenye mstari usemao: I don’t give a damn if you used to talk to Jay Z.” West pia aliubadilisha mstari usemao: “He ain’t with you, he with Beyoncé, you need to stop actin’ lazy” na kusema “You need to stop actin’ crazy.” Pia aliondoa jina la Jay kwenye wimbo Touch the Sky.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents