Burudani

Beef ya Lil Wayne na Birdman kwisha?

Rapa asieishiwa na fujo kila wakati kutokea Marekani Lil Wayne ameamua kumchkoza upya CEO wa “Cash Money”, ambaye ni boss wake wa zamani, Birdman.

Wayne ametumia Instagram yake kwa kupost picha alizopiga na watoto wa boss wake wa zaman Birdman alizopiga nao siku ya ijumaa.

Picha zote ziilizopostiwa ziladikwa “#4L #BLOODLOVE.” kufuatia picha hizo kupostiwa baadhi ya comment zimedai kuwa huwenda Birdman alikuwepo humo ndani japo hakuna ushahidi.

Mpaka sasa bado haijajulikana kama Wayne na Birdman wamemaliza beef lao ama bado. Siku chache zilizopita, Wayne alitangaza kua amejiunga na Roc Nation ya Jay Z mwezi wa kumi, mwaka jana.

Wayne alimtusi sana boss wa Cash money wakati wa kilele cha ugomvi wao na mpaka sasa kuna kesi ya madai iliyofunguliwa na Wayne kwa madai ya kiasi cha dola milioni 51.

Licha ya yote hayo, Lil Wayne mara kadhaa alikuwa bado akisema Birdman ni kama baba yake.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents