Burudani

Beka wa Yamoto Band anashikiliwa na Jeshi la Polisi

Msanii wa Bongo Flava, Beka Flavour anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini katika kituo cha Tabata Dar es Salaam kwa tuhuma za kutapeli kupitia mtandao.

Taarifa za awali kutoka kwa mtu wa karibu wa msanii huyo zinaeleza kuwa Beka ameshikiliwa kuanzia saa tano asubuhi baada ya kijana mmoja kuripoti kutapeliwa katika mtandao wa facebook kupitia jina la msanii huyo.

Jitihada za kumtoa zinaendelea kufanywa na watu wake wa karibu na muda si mrefu Bongo5 itakuja na taarifa kamili.

Beka Flavour alifanya vizuri akiwa ndani ya kundi la Yamoto Band kabla ya wasanii wa kundi hilo kuanza kufanya kazi za solo project, na sasa anafanya na vizuri na wimbo wake ‘Libebe’.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents