Michezo

Beki mpya wa Azam FC aanza kujifua rasmi

Mchezaji mpya wa klabu ya Azam FC, Daniel Amoah, ameanza rasmi mazoezi akijiweka sawa na mechi zijazo za timu hiyo.

IMG_2379
Amoah (kushoto) akijifua na Salum Abubakar ‘Sure Boy’

Amoah aliyesajiliwa mwanzoni mwa mwezi huu akitoka Medeama ya Ghana, aliwasili nchini Jumanne iliyopita mara baada ya kuweka mambo yote sawa nchini kwao huko.

Beki huyo katika majukumu ndani ya timu yake hiyo mpya, atakuwa akitumia jezi namba tatu mgongoni iliyokuwa ikitumiwa na kipa Ivo Mapunda aliyesitishiwa mkataba mwishoni mwa msimu uliopita.

Kuwasili kwa Amoah kunazidi kukiimarisha kikosi cha Azam FC katika idara ya ulinzi hasa baada ya kutokuwa kikosini kwa mabeki wa kati Aggrey Morris na Pascal Wawa, ambao wako kwenye programu ya mwisho ya kutibu majeraha yao ya goti.

Moja ya sifa kubwa za Amoah ni uwezo kukabiliana na washambuliaji wasumbufu akitumia akili na nguvu, ambapo ni mmoja wa wachezaji waliochangia mafanikio ya Medeama kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka huu.

Beki huyo, 18, pia ana uwezo wa kufunga mabao ambapo mpaka sasa ameifungia mabao matatu Medeama, kwenye Ligi Kuu ya Ghana akifunga mawili na moja katika Kombe la Shirikisho.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents