Burudani ya Michezo Live

Beki wa Liverpool Gomez awa sababu ya mchezaji wa Man City Raheem Stearling kutolewa timu ya taifa – Video

Beki wa Liverpool Gomez awa sababu ya mchezaji wa Man City Raheem Stearling kutolewa timu ya taifa - Video

Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester City Raheem Sterling ameondolewa katika Kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kinachojiandaa dhidi ya Montenegro katika kufuzu michuano ya Euro 2020kwa kosa la ugomvi.


Kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza amefafanua kuwa wamelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kuzuka ugomvi baina ya Raheem Sterling na Joe Gomes katika uwanja wa mazoezi wa St. George’s Park.

Ikumbukwe Sterling wa Manchester City, alitunishiana kifua na beki wa Liverpool, Joe Gomez, wakati wa ushindi wa Liverpool 3-1 huko Anfield Jumapili. Chama cha Waandishi wa habari England, kimeripoti kuwa wawili hao walizusha tafrani tena siku ya Jumatatu wakati wa mazoezi ya timu ya England.


Kocha wa England, Southgate amesema: wamechukua uamuzi wa kutomjumuisha Raheem kwenye mechi dhidi ya Montenegro Alhamisi, na uamuzi huo umefanywa kwa makubaliano ya kikosi kizima cha England.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW