Michezo

Beki wa Tottenham ang’atwa na panya mguuni Afrika Kusini ‘Alitengeneza shimo kubwa mguuni kwangu’

Aliyekuwa beki wa klabu ya Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya Uingereza, Gary Mabbutt amesema kuwa amelazimika kurejea haraka nchini kwao kufuatia sehemu ya mguu wake kuliwa na panya nchini Afrika Kusini alipokuwa kwenye likizo.

Mabbutt amesema kuwa tukio hilo limemfika wakati alipo mtembelea binti yake ambaye anafanya kazi kwenye mbuga ya wanyama ya taifa ya Kruger wiki sita zilizopita na kumlazimu kuwa hospitali nchini Uingereza kwa zaidi ya siku saba.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Telegraph kimeeleza kuwa nahodha huyo wazamani wa Tottenham mwenye umri wa miaka 57 anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na ahisi maumivu mwilini mwake hivyo haikuwa rahisi kufahamu tukio hilo likitokea mpaka alipoamka.

“Nilikwenda kulala na nyakati za usiku panya alikuja chumbani kwangu, alipanda kwenye kitanda na kuamua kula mguu,” amesema Mabbutt.

“Alitengeneza shimo kubwa mguuni kwangu, kuelekea ndani kabisa ya mfupa na kula ndani kabisa. Mwanangu alipokuja chumbani aliniambia baba kuna kitu kimekupiga, ukiwa Afrika unafikiria kuwa ni nyoka na nge.”

“Kwa bahati nzuri panya huyo alikula vizuri kiasi kwamba sikuweza hata kuhisi kitu chochote kile.”

Beki huyo wa zamani wa Tottenham kila siku anaendelea kwenda hospitali kupata matibabu ili kupona majeraha yake.

Related Articles

2 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents