Michezo

Beki wa Tottenham awaniwa kama mpira wa kona, Chelsea wajitosa kwa Cavani, wengine sokoni

Chelsea imetoa ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay, Edinson Cavani, 32, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Times)

Edinson Cavani

Babake Cavani amesema nyota huyo atajiunga na Atletico Madrid ikiwa klabu hiyo ya Uhispania itaafikiana na PSG. (Guardian)

Tottenham wanamlenga mshambuliaji wa Real Sociedad, Mbrazil Willian Jose na kiungo huyo wa miaka 28-anatarajiwa kusafiri London kwa mazungumzo. (AS)

Klabu sita za ligi ya premier zinataka kumsaini beki wa Tottenham Muingereza Danny Rose, 29, mwezi huu. (Sky Sports)

Tottenham wanapanga kutoa ofa ya pili ya kumnunua mshambuliaji wa Fenerbahce na Kosovo Vedat Muriqi. (Aksam, via Sport Witness)Danny Rose

Klabu sita za ligi ya premia zinamng’angania beki wa Tottenham Muingereza Danny Rose

Beki wa Shakhtar Donetsk na Ukrain Mykola Matviyenko, 23, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuenda Manchester City, yuko katika mazungumzo na Arsenal, ajenti wake anasema. (Football.London)

West Ham imeonesha nia ya kutaka kununua winga wa kimataifa wa Ukochi na Bournemouth Ryan Fraser, 25, ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu wa joto. Kiungo huyo pia ananyatiwa na Arsenal na Liverpool. (Mirror)

Everton bado wanamtaka mshambuliaji wa Gremio Mbrazil Everton Soares, 23. (UOL, via Star)Ryan Fraser

West Ham wanataka kununua winga wa kimataifa wa Ukochi na Bournemouth Ryan Fraser

Barcelona wanajitahidi kukamilisha mkataba wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Valencia na Uhispania Rodrigo Moreno, 28, baada ya kumkosa mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (Sport)

Chelsea wanatafakari uwezekano wa kumuuza kipa wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, msimu wa joto, na huenda wakamnunua kipa wa Burnley Nick Pope, 27. (90Min)

Winga wa Uholanzi Tahith Chong, 20, yuko tayari kuondoka Manchester United mwisho wa msimu huu. (Goal.com)Kepa ArrizabalagaChelsea wanatafakari uwezekano wa kumuuza kipa wa Uhispania Kepa Arrizabalaga

Middlesbrough, Stoke na Derby wanasubiri kuona ikiwa Bournemouth itamruhusu beki Muingereza Jack Simpson, 23,kuondoka kwa mkopo. (Sky Sports)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents