Soka saa 24!

Beki wa zamani wa Manchester Patrice Evra ampigia debe Ronaldo katika tuzo za Ballon d’Or

Beki wa zamani wa Manchester Patrice Evra ampigia debe Ronaldo katika tuzo za Ballon d'Or

Aliyekuwa beki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Patrice Evra ameamua kumpigia debe aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Manchester United ambaye kwa sasa amesajiliwa katika klabu ya Juventus Cristiano Ronaldo.

Evra ameamua kuchukua jukumu hilo kupitia akaunti ya Ronaldo baada ya post yake inayomuonesha Ronaldo akionyesha ishara ya kuwapigia makofi na kuwa pongeza mashabiki,huku picha hiyo ikionyesha ilikuwa ni katika mchezo wao dhidi ya Manchester ambapo Manchester alifanikiwa kushinda goli 2-1 ugenini dhidi ya Juventus.

Ikumbukwe kwamba Ronaldo anawania tuzo ya 6 ya mchezaji bora wa dunia,tuzo zinazotolewaga na jarida kutoka nchini Ufaransa, tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwaka huu.

Evra aliandika kuwa ” Usiwe na wivu,ni muda wa kumpatia kile anachostahili Goldengoal namba 6 ”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW