Burudani

Belle 9 amshangaa Ben Pol

Kuonyesha kuwa kitendo alichokifanuya Ben Pol kupiga picha akiwa mtupu ni chaujasiri, Belle 9 amefunguka kuwa hawezi kufanua kitu kama hicho.

Belle amesema hawezi kupiga picha kama hizo kwa kuwa maadili yetu ya kiafrika hayaruhusu kuonyesha kitu kama hicho.

“Kwa maadili ya kiafrika na kwa jinsi ambavyo tumezoea sio kitu cha kawaida ninaweza sema lakini sijui labda anaweza akaja kutengeneza sababu ambazo zitaendana na zile picha. Kiukweli mimi siwezi, Siamini katika hilo kuwa muziki wa Ben Pol umeshindwa na upepo ila naona kama ameenda ‘speed’ kidogo. Ben Pol ana ujasiri mkubwa,” muimbaji huyo amekuiambia kipindi cha FNL cha EATV.

Kwa sasa Belle ameachia wimbo wake mpya ‘Ma Ole’ aliomshirikisha G Nako.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents