Burudani

Belle 9 asema haumizwi tena na kutoshinda tuzo

Belle 9 amekiri siku za nyuma, kukosa tuzo kilikuwa ni kitu kilichomsumbua lakini sio sasa.

BELLE 9

Akiongea na E-News ya EATV, Belle alisema kwa sasa kukosa tuzo sio kitu kinachomnyima raha.

“Unajua mwanzo nilikuwa nikijiuliza sana juu ya vigezo vinavyomwezesha msanii kutuzwa tuzo,” alisema.

“Kila mtu anajua kazi zangu na karibu kila ngoma ninayotoa huwa ni hit song. Sasa hivi kwangu naona kawaida, kwahiyo hata ikitokea sasa hivi kupata tuzo au kutopata, nitafeel kawaida tu. Ila mwanzo ilikuwa ikiniumiza japo ina maana kubwa kwa msanii,” aliongeza.

“Kwa upande wangu naona ni muhimu kuendelea kukomaa kufanya kazi kali na nzuri na huenda labda muda wangu wa kuchukua tuzo haujafika.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents