Burudani

Belle 9 atuhumiwa kuiba wimbo ‘Ma Ole’

Belle 9 atuhumiwa kuiba wimbo wa msanii Tox Star.

Wimbo ambao muimbaji huyo anatuhumiwa kuuiba ni ‘Ma Ole’ aliomshirikisha G Nako ambapo Tox amesema wimbo huo unatokana na wimbo wake ambao alioupa jina la ‘Ole’.

Akiongea na EA Radio katika kipindi cha Planet Bongo, msanii huyo ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo wake ‘Pretty Girl’ aliomshirikisha Alikiba, amesema Belle amecopy kiitikio chote cha wimbo wake huo na pia alichotofautisha katika hilo ni kufanya mdundo wa wimbo huo kwenda haraka tofauti ule wa kwake.

Tox ameongeza kuwa hata ukimsikilizisha mtoto mdogo wimbo huo atakupa jibu. Kutokana na kitendo hicho msanii huyo amesema wimbo wake mpya unaofuata ataupa jina la ‘Masumu ya Mapenzi’ ambapo jina hilo linatoka kwenye wimbo wa mwanzo wa Belle 9 uliomtambulisha kwenye ramani ya muziki miaka kadhaa iliyopita ambao unaitwa ‘Sumu ya Penzi’.

Hata hivyo Bongo5 imemtafuta Belle 9 lakini ameshindwa kuzungumzia lolote kuhusu jambo hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents