Burudani

Ben Pol adai muziki wa Bongo Fleva umeshuka kidogo, awahusisha BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amesema kuwa kwa sasa muziki huo umeshuka kidogo na hii ni kutokana na presha kwa wasanii, vyombo na taasisi za kiserikali zinazosimamia muziki huo.

Related image
Ben Pol

 

Ben Pol amefunguka hayo kwenye mahojiano yake na EATV kwenye kipindi cha Kikaangoni ambapo amedai kuwa

Bongo Fleva na yenyewe kama imetetereka hapa katikati, naona kama kuna presha ya kutoa muziki mzuri, kuna presha ya kuwa relevant, kuna presha ya wasanii wachanga kutoka, kuna presha ya vyombo kama taasisi kumekuwa na presha ambao ndio walezi wetu,“amesema Ben Pol na kuwazungumzia BASATA.

“BASATA ni chombo na chombo pia kinaongozwa na binadmu, hata tukikataa hatuwezi kujikataa kuwa sisi ni binadamu wote sisi ni binadamu. Kunaweza kuwa na makosa ya kibinadamu pia taasisi yoyote au chombo chochote kwa sababu kinaongozwa na binadamu kinaweza kikawa na makosa ya kibinadamu. Naheshimu namna ambavyo wanasimamia na wanapigania sanaa yetu lakini sote ni binadamu.“amemaliza Ben Pol.

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wamekuwa wakilituhumu Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuwa limekuwa likiwakandamiza kwenye kazi zao badala ya kuwasaidia kama wanavyopaswa kufanya.

 

Related Articles

7 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents