Burudani

Ben Pol aeleza kwanini album yake ina nyimbo 20 zikiwemo za zamani

Ben Pol amedai sababu mbili kuu zilizochangia kujumuisha nyimbo 20, kwenye album yake ya kwanza iitwayo ‘Ben Pol’, ni kutokana na kuielekeza kwenye soko la kimataifa pamoja na ubovu wa menejimenti yake ya awali.

Ben Pol akitumbuiza

“Nimeweka nyimbo 20 kwasababu kwanza, hiyo ni album yangu ya kwanza kuipeleka International. Nimeiweka katika mitandao mikubwa kama amazon.com na itunes. Ilinibidi niipe title ya Ben Pol na nijumuishe na nyimbo zangu za mwanzo ambazo hazikuuzwa vizuri kutokana na menejimenti niliyokuwa nayo kipindi cha nyumba kuwa mbovu,” Ben Pol alifunguka kupitia kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Radio iliyopo jijini Mbeya.

“Naamini itanisogeza kwa sababu kila kitu unachokifanya kina makusudi yake na kitakuwa na faida sehemu fulani. Watu wanasapoti muziki, wanataka kununua. Kuna Wabongo wapo nje ambao wananunua nyimbo online, kuna marafiki zetu kupitia raia wa kibongo nao wanapenda kusapoti pia. Kwahiyo ni lazima kuwe na namna ambayo mtu anaweza kuinunua kwa namna moja ama nyingine italeta faida ya kimapato na kujitangaza.”

Katika hatua nyingine Ben Pol amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kusubiria video ya wimbo wake wa Unanichora. Pamoja na mtandaoni, mashabiki wanaweza kuinununua album yake kwa kuwasiliana na namba hizi, 0715744911 na 0764905470.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents