Burudani

Ben Pol afuata nyayo za Wema Sepetu kwenye hili

By  | 

Mkali wa muziki wa RnB nchini, Ben Pol ameteka headline kwenye mtandao wa kijamii wa instagram kwa picha moja ambayo hajaieleweka maana yake nini. Wakati huo akauti yake ya instagram ikiwa na picha hiyo moja tu!, kwa maana kwamba picha za awali zote alifuta.

Ikumbukwe mwaka jana Wema Sepetu alifuta picha zake zote instagram na aliporejea katika mtandao huo January 28 mwaka huu, February 3 alitangaza ujio wa app yake. Mwanamuziki Mwasiti naye aliwahi kufuta picha zote na aliporejea December 13 mwaka jana alitangaza ujio wa wimbo wake mpya ‘Kaa Nao’

Ben Pol nae amefanya kama wao, bila shaka kuna kitu kipya kina kuja kutoka kwake, ila picha aliyoweka kabla hata hatujajua nini kinafuata imezua gumzo na majadala mzito huko wengine wakikosoa vikali picha hiyo. Itazame hapa chini.

Picha aliyopost Ben Pol

Picha hii hadi sasa ina comment 1,607, like 9,393 katika akauti ya instagrama yenye followers million 1.3, facebook comment 303, like zaidi ya 1,400 akaunt yenye watu 239,724.

By Peter Akaro

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments