Burudani

Ben Pol akerwa na wasanii waliomshirikisha kutompa credit kwenye video

Muimbaji wa R&B nchini Tanzania Ben Pol leo Jumatatu kupitia Twitter ameandika:

Baada ya kuona tweet hiyo Bongo5 imempigia simu Ben Pol kupata maelezo zaidi ya hicho alichokisema ambapo amedai kuwa yeye kwake hajakichukulia kama kitu kikubwa sana lakini ni haki yake kupewa credit kwenye kazi aliyoshiriki kwa kuimba mistari kadhaa.

“Lakini nimeona kama sio fair hivi kwasababu mimi mwenyewe nataka exposure kwahiyo kama hujaniita kwenye video unaweza ukaniweka tu, andika tu pale kwenye credit nini kwamba jamaa amefanya kitu. Kidogo inatia faraja kwasababu ni kazi za bure, unafanya for love tu, hamna chochote unacholipwa, lakini atleast hata mtu akikuandika unajisikia kidogo.”

Ben Pol amesema hiyo ni miongoni mwa sababu zinazomfanya aanze kupunguza kufanya collabo siku za hivi karibuni.

“Hiyo ni moja wapo sababu mwisho wa siku unajua kama mtu hata kukuandika hajakuandika maana yake kwako wewe ni hasara, kwasababu yaani unakuwa kama umepoteza lakini atleast mtu kama hajakulipa lakini akakuandika kwenye credit ile nyimbo inaweza ikaenda mbali, wewe ikakusaidia ukapata opportunity zingine kubwa kama mtu amekuandika hata credit, lakini kama credit hujaandikwa maana yake ile nguvu yako pale ambapo umefanya ni loss.”

Miongoni mwa watu waliovutiwa na tweet ya Ben Pol ni Fid Q ambaye amemwambia:

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents