Burudani

Ben Pol apanga kujitoa kwenye biashara ya miito ya simu ‘ni aibu kutaja kiasi nilichowahi kuingiza’

Ben Pol amesema atajitoa rasmi kwenye biashara ya miito ya simu ‘RBT’ baada ya kudai imekuwa biashara kichaa kwake kwa miaka minne sasa.

Ben Pol

Ben Pol amesema hata kwenye malipo hayo ambayo amedai ni aibu kuyataja hupatikana mpaka mfikishane kwenye vyombo vya dola.

“Nimeachana na RBT kwasababu haijawahi kunilipa vizuri ni kama biashara kichaa kabisa.” Ben ameimbia Bongo5.

“Halafu pia ukichukia hatua let’s say za kisheria ndio unaweza kuona ripoti za mauzo nini, ndio watu wanakuletea,lakini hivi hivi wanakuwa wanasumbua sana. Hii ni kwangu mimi sijui kwa wenzangu. Kwenye RBT nimeingiza nyimbo zangu zote ,isipokuwa Jikubali,Pete na Unanichora ndio nyimbo ambazo sikuingiza. Pesa ambazo wamenilipa kwa nyimbo zangu nyingine nikisema nizitaje itakuwa aibu.”

Kutokana na ukweli huo, Ben Pol amesema yupo kwenye maandalizi ya kuandika barua ili waziondoe nyimbo zake.

“Kwenye kampuni zote ambazo nimefanya nazo biashara hii naenda kutoa nyimbo zangu,sasa hivi nipo kwenye kuandaa barua halafu nasitisha kwenye kampuni zote,halafu naweza nisiuze tena.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents