Burudani

Ben Pol asema mama yake alimlea kwa biashara ya vitumbua baada ya baba yake kufungwa jela miaka 2

Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol amesema kuwa Baba yake mzazi alifungwa kifungo cha miaka miwili wakati mama yake mzazi akiwa na ujauzito wake.
Ben Pol

Ben Pol amekiambia kipindi cha 5 Selekt cha EATV kuwa hali hiyo ilimfanya Mama yake afanye biashara ya maandazi na vitumbua ili amudu gharama za maisha.

“Unajua mimi najua nilipotoka mpaka nilipofika hapa naweza kusema I made it, wakati mama yangu ana ujauzito wangu wa miezi sita baba yangu mzazi alifungwa jela miaka miwili hivyo mama alipambana kwa kuuza maandazi na vitumbua mpaka nazaliwa na kunilea hivyo leo kwa hapa nilipofika huwa napenda kushare historia yangu ili watu wajue,” alisema Ben Pol.

Mbali na hilo Ben Pol anasema kuwa yeye hakuzaliwa hospitali bali mama yake mzazi wakati wa kumzaa yeye alijifungua akiwa nyumbani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents