Burudani

Ben Pol awashukuru mashabiki wa mapokezi ya kishindo

MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul ‘Ben Pol’ ameshukuru mashabiki kwa Kumpa ushirikiano kila anapotoa nyimbo yake mpya, huku akiwataka waupokee wimbo wake mpya inaitwa Hiyo ndio Mbaya.

Alisema amekuwa akipata ushirikiano hivyo ujio wa muziki wake huo aliutoa kwa staili ya Singeli.

“Nashukuru kwa support ninayopata kutoka kwa mashabiki zangu na wadau , sasa nina miaka 10 kwenye muziki wamekuwa na mimi bega kwa bega, sasa nimekuja na wimbo singeli unaitwa “Hiyo ndio Mbaya” ambao nimemshirikisha msanii mpya Tamimu, studio tumefanyia Pizzey Records, Producer ni Jay Stereo, katika kufunga mwaka nitatoa wimbo mpya kila wiki, mashabiki zangu wajiandae kupokea kazi zangu’alisema Pol.

Pia nimeanza kuzunguka mikoani kufanya matamasha ya kuwashukuru mashabiki zangu nimeanzia Mbeya , mikoa mingine inafuata naomba wanipokee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents