Burudani

Ben Pol kusafiri nchi za Ulaya kufanya utafiti wa masoko ya muziki wake

Msanii wa Rnb Ben Pol amesema hivi karibuni anatarajia kusafiri nchi za Ulaya kwa lengo la kwenda kufanya utafiti juu ya masoko ya muziki wake akianzia nchini Denmark.
ben

Akizungumza na bongo5 leo Ben Pol amesema utafiti huo utamsaidia kujua jinsi ya kuwafikishia mashabiki wake wa nje kazi zake kwa muda muhafaka, na kuongeza kuwa anatarajia kusafiri kuanzia November mwaka huu.

“Itakuwa tour ya research ambayo itanipa matokeo ya muzuki wangu kwa nchi za nje pamoja na hayo nitafanya wimbo nikiwa kwenye hiyo tour,na pia nitapata mambo mengi sana kama nilivyo sema nafanya research kwahiyo mengi yataibuka tumuuombe mungu”.Alisema Ben Pol

Wakati huo huo Pol amewalalamikia matapeli wa mtandaoni ambao wameingia katika account zake za facebook na kuwatapeli watu, hali iliyomfanya kuwapa tahadhari fans wake juu ya ‘hackers’ na kuwashauri fans wake wakiona dalili yoyote ya utapeli kuwa block.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents