Burudani

Ben Pol: Nipo tayari kurudi tena shule

Muimbaji wa ‘Sophia’ Ben Pol amedai kuwa kwa sasa yupo tayari kurejea shule.

10471830_1067608546598577_1170745707_n

Ben aliwahi kuwa mwanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha, IFM lakini hata hivyo hakuweza kumaliza masomo.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, msanii huyo amedai kuwa hakuacha shule kama watu wanavyodhani bali aliahirisha mwaka kwa matarajio ya kuja kurejea tena baadaye.

Amedai kuwa hivi karibuni amekuwa akiangalia mbadala wa kusoma Open University. Ben anadai anaona sasa anaweza kuendelea tena na masomo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents