Burudani

Bendi ya Msondo Ngoma yataka ilipwe na WCB milioni 300 kisa ‘Zilipendwa’

Hii ni habari mbaya kwa kambi ya WCB inayoongozwa na Diamond kama ni ya kweli, kwani wanasheria wa Bendi ya Msondo Ngoma ametaka mteja wao kulipwa tsh milioni 300 na WCB kwa madai wametumia kionjo cha melody ya saxaphone cha wimbo wa bendi hiyo bila hurusa katika wimbo wa WCB, ‘Zilipendwa’.

Alhamisi hii zilianza kusambaa barua mtandaoni zikidaiwa kutoka kampuni ya sheria ya bendi hiyo, Maxim Advocate huku barua hiyo ikionekana kupitia Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) pamoja na COSOTA.

 

Bado WCB hawajazungumza chochote kuhusu tukio hili. Angalia barua hizo hapa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents