Michezo

Benitez akubali kuendelea kubaki Newcastel United

Kocha wa klabu ya Newcastel ya nchini Uingereza, Rafael Benitez amekubali kubaki kuifundisha timu hiyo iliyoshuka daraja msimu huu.

IMG_9379

Benitez alisajiliwa kuifundisha timu hiyo mwezi Machi akiwa kama kocha huru ili kuiokoa timu hiyo isishuke daraja lakini hali ilikuwa mbaya zaidi hatimaye mwisho wa msimu huu ilishuka daraja kwa kushinda mechi ya mwisho magoli 4-1 dhidi Spurs.

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari leo, Benitez ambaye ana mkataba na timu hiyo wa miaka mitatu amekubali kuendelea kuifundisha timu hiyo ili kujaribu kuirudisha kucheza ligi kuu ya Uingereza kwa msimu wa mwaka 2017-2018.

Hata hivyo timu hiyo iliwahi kushuka daraja kwa msimu wa mwaka 2009-2010 na kufanikiwa kurudi kucheza ligi kuu msimu uliofuata.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents