Habari

Benki ya NMB yaja na huduma tatu za kidijitali, sasa utafungua akaunti ya benki kupitia simu ya mkononi

Katika kukabiliana na ushindani na kasi ya mabadiliko ya teknolojia nchini, Benki ya NMB Plc imeingiza sokoni huduma tatu kwa mpigo za kibenki kidijitali ikiwemo ya kufungua akaunti ya benki ndani ya dakika tatu kwa kutumia simu ya mkononi.

Huduma hizo tatu zilizozinduliwa ni uwezo wa mwananchi kufungua akaunti kupitia simu yake ya mkononi, App yenye huduma zote ambazo mteja anaweza kufanya mwenyewe badala ya kwenda kwenye tawi na huduma ya Scan to Pay huduma ya kufanya malipo kwa kutumia QR code. App ya NMB KLiK inapatikana katika Playstore https://goo.gl/Fr9fZf na kupitia AppStore https://goo.gl/wQXZV6

https://youtu.be/wrwNLBmn8a0

Mkuu wa Idara ya Ubunifu wa benki hiyo, Josina Njambi amesema huduma tatu zilizozinduliwa zinajumuisha namna mpya ya kujiunga na benki (accessebility), namna mpya inayomwezesha mteja kutumia benki yake kikamilifu kidijitali na huduma ya tatu inalenga zaidi kujenga jamii isiyotegemea pesa za mifukoni (Cashless society).

Njambi amesema huduma hizo zitakuwa zinafuata nguzo tano ambazo ni kufikiwa kwa urahisi popote ulipo Tanzania, kurahisisha huduma za benki hiyo kwa wateja wake, huduma za haraka, iliyosalama na huduma kutokana na mahitaji ya wateja.

Kwa wanaotumia simu janja maarufu kama smartphone, huduma hizo zinapatikana katika programu ya simu iitwayo NMB Klik wakati wale wenye simu za kawaida zilizopewa jina la utani za “Vitochi” watatumia ujumbe mfupi wa maneno (Shortcode Sms).

Katika mabadiliko hayo, Njambi amesema wateja wa benki hiyo wanapofungua akaunti hawatalazimika kutumia “fomu za makaratasi, kulipia gharama za kufungulia, masharti ya kuchosha na wala hawatahitajika kufika katika tawi la benki”.

“Mtu anayetaka kufungua akaunti atahitajika kuwa na moja ya vitambulisho vya aina tano ambavyo ni leseni ya gari, kitambulisho cha taifa, kitambulisho cha kupigia kura, pasi ya kusafiri na kitambulisho cha Mzanzibari mkazi mteja wa benki ya NMB ataweza kutumia kitambulisho kimoja wapo kufungulia akaunti kupitia simu kwa kuboonyeza *150*66# kujiunga.

Uzinduzi huo uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt umehudhuriwa na Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Benard Kibese ambaye alisema kwamba ubunifu huo utarahisha Watanzania wengi kufungua akaunti za benki hiyo kupitia simu zao za mikononi na kwamba hivi sasa watumiaji wa simu za mkononi ni wengi na hivyo huduma hiyo ya NMB imekuja wakati sahihi.

β€œTunaipongeza NMB kwa ubunifu huu ambao wamekuja nao wa kuhakikisha wanatumia teknolojia iliyopo kuanzisha huduma za kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi na kizuri zaidi hata wenye simu za tochi bado wanaweza kufungua akaunti kupitia huduma hiyo,” amesema Dk. Kibese.

Huduma hiyo imepokelewa vizuri na watumiaji wa mtandao wa Twitter ambao wamesema kwamba uzinduzi huo ni muhimu sana hususani katika mchakato wa kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa kati.


https://twitter.com/PatNanyaro/status/1029317002589024258

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents