BurudaniHabari

Benki ya NMB yanogesha Siku ya Kizimkazi Zanzibar!

Benki ya NMB inaendelea kuboresha miundombinu na mazingira ya shule visiwani Zanzibar kwa kutoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi Milioni 10/- zilizofanikisha ujenzi wa vyoo vyenye matundu 10 katika shule ya Kibuteni iliyopo Wilaya ya Kusini. NMB pia imetoa tisheti 300- ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono sherehe za Kizimkazi ‘Kizimkazi Day’ zinazofanyika kila mwaka mwezi wa nane – Lengo ikiwa ni kutathmini shughuli za kimaendeleo katika maeneo ya Kizimkazi na kuangali changamoto zilizopo ili kuzipatia utatuzi.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam- Donatus Richard alipotembelea akina mama wajasiriamali wanaodhaminiwa na Benki hiyo kwenye hafla ya Kizimkazi Day Wilaya ya Zanzibar. Akishuhudia ni Meneja Masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii – Bi Lilian Kisamba (mwenye koti)

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Maafisa wa Benki ya NMB katika hafla ya kukabidhi msaada wa vyoo vya matundu 10 vyenye thamani ya sh. Milioni 10/- kwa shule ya Msingi Kibuteni iliyopo Zanzibar Wilaya ya Kusini.

 

Jengo la choo cha matundu 10 lililokabidhiwa na Benki ya NMB kwa matumizi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kibuteni Zanzibar Wilaya ya Kusini.

Siku hii huratibiwa na Makamu wa Rais- Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wa Serikali visiwani humo. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mheshimiwa Samia ameishukuru Benki ya NMB kwa namna inavyokuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii mbalimbali kama Elimu, Afya na Maafa.

Ni miaka mingi sasa, Benki ya NMB imekua ikitoa asilimia 1℅ ya faida yake kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayowanzunguka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents