Habari

Benki ya NMB yatoa elimu ya matumizi makini ya fedha na jinsi ya kuweka akiba kupitia benki hiyo kwa wananfunzi

Wanafunzi wafaidika na elimu ya kuweka akiba kupitia Benki ya NMB

Katika kutambua umuhimu wa vijana ambao ni Taifa la kesho, Wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya Wasichana ya Barbro Johansson Model iliyopo jijini Dar es Salaam, wamepata elimu ya fedha na umuhimu wa matumizi makini ya fedha ikiwemo kuweka akiba benki, walipotembelea Makao Makuu ya benki hiyo kujionea shughuli mbalimbali za kibenki kwa vitendo.

Wanafunzi wakipata elimu kutoka kwa Maofisa wa benki ya NMB- Monica Job(kushoto) na Subira Kapita (Kulia)

Wanafunzi hao walipata nafasi ya kujifunza na kutembelea idara na vitengo tofauti ili kufahamu shughuli zao lakini pia walitembelea Tawi la NMB Ohio.

Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna akikata keki pamoja na wanafunzi.

Pamoja na hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amewaasa wanafunzi hao kuwekeza nguvu zaidi katika elimu, kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

Wanafunzi wakifurahi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa NMB- Ruth Zaipuna na Mwalimu wao- Jennifer Dominick.

Baada ya mafunzo hayo, wanafunzi wote walipata nafasi ya kufungua akaunti zitakazowawezesha kutunza fedha na kujijengea tabia ya kuweka akiba na kunufaika na huduma na bidhaa za benki ya NMB hususan Chipukizi na Mwanachuo Akaunti.

#NMBkaribuyako.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents