Michezo

Bernard Arthur: Azam FC watarajie kama niliyofanya Ghana

Mshambuliaji mpya wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Bernard Arthur, amewasili rasmi nchini jana siku ya Jumapili akitokea Ghana.

Mara baada tu ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere , Arthur ameweka wazi kuwa amekuja kuisaidia timu hiyo kumaliza kwenye nafasi nzuri Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ikiwemo kutwaa ubingwa.

“Malengo yangu ni kujiunga na kuendeleza niliyofanya nchini Ghana kwa kuyaleta hapa natarajia mambo mazuri kama kila kitu kitakwenda vizuri kama unavyojua mambo ya mpira wakati mwingine kuna kupanda na kushuka yote haya ni fomu si unajua namna ya kuipata fomu.

“Nitajitahidi kujiweka vizuri, kufanya mazuri kwa klabu na kufanya mazuri binafsi, kufunga mabao kadhaa kama sitofunga basi angalau kutoa pasi nzuri za mabao na kuisaidia klabu kuwa kwenye nafasi nzuri na kutwaa taji la ligi,” amesema Arthur.

Arthur amesema anasmhukuru Mwenyezi Mungu kwa kufanikiwa kujiunga na klabu bora ya Azam FC huku akidai hiyo ni njia sahihi ya kufikia malengo yake.

“Kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kufika salama Tanzania na najisikia vizuri kujiunga na klabu hii ya ajabu yenye baadhi ya historia nzuri. Nimeijua Azam FC kupitia wachezaji wenu Yakubu (Mohammed), Razak (Abalora) ambao ni rafiki zangu mmojawapo nilicheza naye Razak wameniambia kuhusu timu hii.

“Ofa ilipokuja sikujiuliza chochote kuhusu kujiunga nayo, nafikiri kujiunga na Azam FC ni jambo zuri kwangu na zuri kwa kipaji changu na maendeleo yangu na timu pia,”.

Mshambuliaji huyo anaesifika kwa kushambulia kwa spidi, kupiga mashuti, kufunga mabao na kusumbua mabeki, amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 11 kwenye msimu ulioisha wa Ligi Kuu Ghana (GPL), ambapo mbali na kuichezea Liberty pia amewahi kupita WAFA SC ambayo iliwahi kumpeleka kwa mkopo kwa vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents